WAPINZANI WA YANGA WAWASILI NCHINI TAYARI KWA MECHI

Timu ya Ngaya FC  Comoro tayari wameshawasili hapa nchini kwa ajili ya mechi yao ya marejeano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Yanga hapo siku ya jumamosi.

Katika mechi ya kwanza wakikilishi wa Tanzania katika michuano hiyo timu ya Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 wakiwa ugenini huko Comoro hivyo kufanikiwa kuwa na mtaji mzuri wa mabao.
Yanga katika mechi hiyo inahitaji ushindi wowote ama sale au kutoruhusu kufungwa zaidi ya magoli matatu ili wafanikiwe kufuzu katika hatua inayofuata ambapo hatua hiyo huenda wakakutana na APR ya nchini Rwanda ama Zanaco ya Zambia.

No comments