KVZ WAMEFIKA SALAMA BUJUMBURA, CAPTAIN WAO ASEMA SASA KAZI KAZI TU JUMAMOSI

Na:Sleiman ussi haji Zanzibar .
Wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika timu ya KVZ jana imewasili salama Bujumbura Mjini Burundi wakitokea Jijini Dar es salam kwa Basi moja kwa moja kwenda huko kwa ajili ya kucheza na wenyeji wao timu ya Messager Ngozi kwenye mchezo wa marejeano wa Shirikisho utakaofanyika kesho kutwa Jumamosi ya Februari 18, kuanzia saa 10:00 za huko na kwa Tanzania ni Saa 9:00 za mchana.
Kwa mujibu wa Captain wa timu hiyo Suleiman Abdi (Sele Tz) amesema wamefika salama jana saa 12 za jioni na wamepewa huduma zote nzuri na wenyeji wao.
“Tumefika salama hapa Bujumbura jioni jana na tunashukuru wenyeji wetu wametupokea vizuri na wanatupatia huduma nzuri sana, tumewekwa kwenye bonge la Hoteli, huduma zote nzuri zimo huku kwenye Hoteli, tunawaomba Wazanzibar watuombee dua sisi tutapigana kufa kupona huku”. Alisema Sele Tz.
Katika msafara uliokuwepo huko una jumla ya watu 28 wakiwemo wachezaji 19 pamoja viongozi 9
Wachezaji hao ni Yakoub Bakari Juma, Abdallah Suleiman Bakari, Saleh Rajab Nassor, Makarani Miluchu Makarani, Rashid Omar Rashid, Hamid Salum Saleh, Said Issa Mohd, Iddi Mgeni Mrisho, Suleiman Abdi Juma, Seif Said Seif na Mohd Nassor Maulid.
Na wengine ni Suleiman Hassan Ali, Masoud Abdallah Masoud, Sultan Said Kaskas, Maulid Fadhil Ramadhan, Abdallah Suleiman Bakari, Nassir Bakari Iddi, Salum Songoro Maulid na abas suliman bakar.
Viongozi walikokuwepo huko ni Sheha Khamis (Kocha Mkuu), Ramadhan Hussein (Kocha Msaidizi), Mohd Omar Makame, Juma Lugoha Songwa, Hassan Omar, Ramadhan Sheha “Tshabalala” (Msemaji), Juma Hussein (Dokta), Saimon Charles na Rashid Tamim Halfan (Mjumbe wa ZFA).
Mchezo huo utapigwa kesho kutwa Jumamosi ya Februari 18, katika uwanja wa Prince Luic Rwaga Sore huko Bujumbura Mjini Burundi kuanzia saa 10:00 za huko na kwa Tanzania ni Saa 9:00 za mchana ambapo Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Jumapili iliopita Amani Mjini Unguja wenyeji KVZ waliifumua Messager Ngozi kwa mabao 2-1 ambapo katika mchezo wa marejeano KVZ wanalazimika kupata japo sare ili kusonga mbele katika hatua nyengine.

No comments