MABWEPANDE WAANZA MCHAKATO WA KUIBUA VIPAJI VYA WACHEZAJI

Katika kuhakikisha kuwa Kata ya Mabwepande iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam inaendelea kwenye sekta ya michezo,wakazi wa sehemu hiyo wameamua kuanzisha timu ambayo itakuwa na mwendelezo mzuri kwa ajili ya kuibua vipaji vya wachezaji ndani ya kata hiyo.

Kwa mujibu wa mdau wa soka ndani ya kata hiyo, Mujuni Lutembeka ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kwa kuonyesha kuwa wamedhamiria kufanya zoezi hilo wameamua kuanzisha timu inayojulikana kama Socer City iliyopo maeneo ya mji mpya ambayo huwa wanatumia uwanja mpya kwa ajili ya mazoezi

Lutembeka alisema kwamba bado wakazi wa kata hiyo hawajaanza kuifahamu vizuri timu hiyo,hivyo kwa sasa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanawafahamisha wakazi wa maeneo hayo ili kufahamu namna ya kuisaidia Mabwepande nayo ijulikane katika ramani ya soka.

Alisema kuwa mbali na kuibua vipaji vya wachezaji lakini pia wana lengo la kuwapa fursa vijana ili kuepukana na utumiaji wa madawa ya kulevya kama ilivyo kwa serikali inavyopinga utumiaji wa madawa hayo ambayo ni athari kubwa kwa jamii na nchi kwa ujumla.

No comments