TAMKO LA SERIKALI MCHEZO WA SIMBA NA YANGA
Ndugu Watanzania Jumamosi, tarehe 25/02/2017 saa 10.00
jioni Uwanja wa Taifa tutakuwa na mchezo mkubwa wa kati ya Simba SC na Yanga
FC.
Ikumbukwe kuwa mchezo uliopita wa timu hizi uliochezwa
kwenye uwanja huu tarehe 1/10/2016 zilitokea vurumai zilizosababisha Serikali
kuufungia Uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu.Vurugu hizo zilisababisha uharibifu
wa miundombinu ikiwemo uvunjifu wa viti,mageti na mbaya zaidi baadhi ya watu
walijerehuliwa.
Tunaomba waandishi na wadau wote tushirikiane kuelimisha
umma wa wapenda michezo kuwa Michezo ni Furaha, Amani na Upendo.
Kuelekea mchezo ujao tungependa kueleza yafuatayo:-
Tunawaomba wadau wote tujenge utamaduni wa kununua tiketi
mapema kwani mpaka sasa tiketi zinapatikana kupitia SELCOM. Hii itaondoa
msongamano na lawama zisizo za lazima.
Tujiepushe na vurugu za aina yoyote siku ya mchezo kwani
Serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayepelekea uvunjifu wa amani siku ya
mchezo.
Kutakua na ulinzi wa kutosha ndani na nje ya Uwanja hasa
ukichukulia kuwa kuna kamera zenye uwezo wa kumuona kila mtu anayeingia
Uwanjani na kila anachokifanya.Tutapiga picha na kuzirusha kwenye TV kubwa ya
Uwanja kwa wale wote watakaobainika kuashiria/kutenda vurugu sheria itachukua
mkondo wake.
Tunatoa rai kwa waamuzi
waliopewa dhamana ya kuchezesha mchezo huu,wajue kuwa wana dhamana kubwa hivyo
ni vyema wakafuata kanuni na sheria za mchezo husika ili kuepusha malalamiko.
Mwisho napenda niwatakie mchezo mwema kwa timu zote wajue
kuwa Watanzania wanategemea burudani nzuri kutoka kwao,na niwaombe mashabiki
wakumbuke kuwa wajibu wao mkuu ni kuzishangilia na kuzipa hamasa timu zao na si
vinginevyo.
Post a Comment