KUWAONA YANGA NA NGAYA NI SH 3000

Kiingilio cha chini katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika kati ya  Yanga dhidi ya Ngaya ya Comoro ni shilingi elfu tatu kwa viti vya mzunguko huku kiingilio cha juu kikiwa ni shilingi elfu 20 kwa viti vya VIP.

Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa shilingi elfu 10 ambapo milango ya uwanja wa Taifa inataraji kuanza kuwa wazi kuanzia mishale ya saa tano asubuhi au saa sita mchana.

Afisa Masoko wa Yanga,Omary Kaaya amesema kwamba uongozi umeamua kuweka viingilio hivyo ili kuwapa fursa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kulishuhudia pambano hilo linalotarajiwa kupigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments