ZIMAMOTO BADO WAPO SAFARINI KUWAFUATA FERROVIARIO DE BEIRA

Na: Sleiman ussi haji  Zanzibar
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Zanzibar ambao pia ni wawakilishi wa Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Zimamoto bado haijafika Beira kwasasa ipo Maputo na kesho asubuhi wakitarajia kuanza safari kwenda Mjini Beira ambako ndiko kutakapopigwa mchezo wao siku ya Jumamosi.
Timu hiyo iliwasili hapo Maputo Mjini Msumbiji jioni ya leo ambapo jana usiku walifikia Ethiopia na wakalala huko kabla ya leo kwenda hapo na ambapo jana saa 9 za mchana walitokea Zanzibar kwa Ndege ambapo kwasasa wamepumzika katika Hoteli ya Matola na kesho asubuhi kupanda Ndege tena kwenda Beira ambapo watachukua Saa 1 njiani kufika huko kutakopigwa mchezo wao siku ya Jumamosi dhidi ya wenyeji wao timu ya Ferroviario de Beira.
Mtandao huu umezungumza kwa njia ya simu na mlinda mlango namba moja wa timu hiyo Mwinyi Iker na kusema kuwa bado wanaendelea na safari lakini kwasasa wamepumzika wapo Maputo.
“Tupo Maputo sasa tumepumzika mana ndo kwanza tumefika saa 10 ya jioni ya leo, jana usiku tulifikia Ethiopia tukalala leo ndo tumeingia hapa Maputo jioni, kesho Asubuhi tunaenda Beira”. Alisema Mwinyi.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Jumamosi iliyopita Amani Mjini Unguja wenyeji Zimamoto waliifunga Ferroviario de Beira kwa mabao 2-1 ambapo katika mchezo wa marejeano Zimamoto wanalazimika kupata japo sare ili kusonga mbele katika hatua nyengine ya kombe hilo kubwa kwa vilabu barani Afrika.

No comments