SIMBA WAFICHA KAMBI YA TIMU HIYO

Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam umeshindwa kuweka bayana sehemu ambayo kikosi cha timu hiyo kinafanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Meneja wa Simba Mussa Hassani Mgosi amesema kwamba kwa sasa hawatarajii kuweka wazi mipango yao ya mazoezi kwani ni kipindi cha kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mzunguko wa kwanza wa ligi huku wakitaraji kuwa na hali ya utulivu.

"Nadhani taarifa rasmi zitatolewa na viongozi husika hasa msemaji wa klabu Haji Manara juu ya kambi ilipo au tunafanyia wapi mazoezi lakini kwa sasa hatuwezi kuweka mambo yetu hadharani"alisema Mgosi.

Katika hatua nyingine Mgosi amesema kwamba mipango yao ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara iko pale pale kwani msimu huu wamedhamiria kufanya hivyo ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

No comments