KAMPUNI YAJITOKEZA KUIDHAMINI MBAO FC

Kampuni ya Hawai Product imeingia makubaliano na timu ya Mbao Fc kwa ajili ya udhamini wa timu hiyo, mkataba wenye thamani ya shilingi milioni 25 kwa mzunguko wa pili pekee.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,meneja wa masoko wa kampuni hiyo inayoratibu maziwa ya cowbel Elisharia Ndeka amesema kwamba wameamua kutoa udhamini kwa klabu hiyo baada ya kurizishwa na kiwango chao katika ushiriki wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Nae mwenyekiti wa Mbao FC ya Ilemela jijini Mwanza Solly Zephania ameishukuru kampuni hiyo kwa kufanikisha udhamini huo kwani kwa mujibu wa taarifa yake utakuwa na tija kwao hasa katika maswala ya uendeshaji wa timu.

Amesema kwamba udhamini huo wa shilingi milioni 25 unaweza kuongeza mara baada ya miezi sita kumalizika endapo timu hiyo itaendelea kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments