AVEVA AWAITA VIONGOZI WA MATAWI

Rais wa klabu ya Simba  *Evans Aveva* atakuwa na Mkutano na viongozi wa matawi ya klabu ya Simba siku ya Jmosi ya tarehe 3-12-2016 saa Nane mchana,kwenye ukumbi wa mikutano wa klabu,uliopo barabara ya Msimbazi jijini Dar es salaam

Mkutano huo ni maandalizi ya Mkutano mkuu maalum wa tarehe 11-12-2016 ambao utafanyika kwenye bwalo la maafisa wa Polisi Ostrebay jijini Dar.

Pamoja na hayo,mkutano wa Rais na viongozi wa matawi,utajadili kwa kina maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini, inayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari uongozi wa klabu hiyo  umewaomba viongozi wote wa matawi kujitokeza bila ya kukosa katika mkutano huo muhimu sana kwa mustakbali wa Klabu ya Simba.

No comments