TFF YAITAKA SIMBA KUWASILISHA NAKALA YA MALIPO YA HASSANI KESSY



Kamati ya katiba sheria na hadhi ya wachezaji inataraji kukutana tena mwishoni mwa wiki hii kujadili swala la mchezaji Hassani Ramadhani Kessy kuhusiana na madai ya klabu ya Simba kwa mchezaji huyo.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba kamati hiyo imeiagiza klabu ya Simba kuwasilisha mkataba halisi ambao walisainiana na mchezaji huyo pia kuleta ushahidi wa utekelezaji wa malipo ya mshahara kwa miezi mitatu kabla mwisho wa mkataba wake uliomalizika mwezi june mwaka huu.

Katika hatua nyingine kamati hiyo ya katiba,sharia na hadhi ya wachezaji mwishoni mwa wiki hii inataraji kujadili maswala mbalimbali ikiwemo swala la wajumbe wa klabu ya Yanga,Ayubu Nyenzi,Salum Mkemi na Hashimu Abdalah ambao hawa kwa pamoja walienguliwa katika mkutano mkuu wa dharura wa klabu hiyo kwa kigezo cha kushindwa kufuata taratibu na kanuni za klabu hiyo.

No comments