MBEYA CITY WASHINDWA KUMTAMBURISHA MRISHO NGASA

Uongozi wa wagonga nyundo wa mkoani Mbeya City umeweka bayana sababu za kutokutangazwa  kwa majina ya wachezaji wapya na wanaoachwa kwenye kikosi cha Mbeya City fc ambao wanatarajiwa kuanza kutumika katika mzunguko wa pili wa ligi kuu tanzania bara 

Meneja wa klabu ya mbeya city  Geofrey Katepa amesema  kwamba kutokana  kocha Kinnah Phiri kushindwa kuwasili jijini Mbeya siku ya jana  ili aweze kutangaza majina hayo ndio sababu pekee ya kushindwa kutangaza kikosi chao.

Katepa amesema kwamba kocha Kinnah Phiri ameshindwa kuwasili kutokana na sababu mbalimbali za kifamilia ambapo sasa anatarajiwa kutua hapa nchini siku ya jumatatu asubuhi na mchana kutangaza majina ya wachezaji wataounda kikosi cha mbeya city katika mzunguko wa pili wa ligi kuu tanzania bara

Uongozi mbeya city ulipanga kutangaza majina ya wachezaji wataoachwa na wachezaji wapya mnamo novemba  30 na kusogeza mbele hadi siku ya jumatatu ambapo kocha   Phiri atawasili hapa nchini asuhuhi akitokea jijini Blantyre nchini Malawi  na kutangaza kikosi chake wakati wa mchana

No comments