WASAGA FC WAMJIA JUU MICHAEL WAMBURA

Uongozi wa timu ya Wasaga Fc ya mkoani Mara inayoshiriki ligi daraja la tatu imewasirisha malalamiko yao katika shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini ikipinga kuenguliwa kwenye mashindano ya ligi mkoa kinyume na utaratibu.

Meneja wa timu hiyo Abuu Masija amesema kwamba licha ya kuwasilisha malalamiko yao TFF lakini bado hawapati ushirikiano wa kutosha juu ya maamuzi ya jambo hilo.

Masija amesema kwamba uongozi wa timu hiyo  hauna inamni na mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mara,Michael Richard Wambura kwa kuwa yeye ndie muhusika mkuu wa swala baada ya yeye kuipa nafasi timu nyingine ambayo imekuwa haina uhalali wa kushiriki michuano hiyo.

No comments