BUSUNGU ATAMBA KUREJESHA KIWANGO CHAKE YANGA

Mchezaji Malimi Busungu amesema kwamba anatarajia kujiunga rasmi na kikosi cha timu ya Yanga siku ya jumanne kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kujiwinda na mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Busungu amesema hatoweza kuhudhuria mazoezi ya siku ya jumatatu kwa kuwa anahitajika kufika Polisi kusikiliza kesi yake baada ya kupata ajari ya gali wiki iliyopita.

Amesema kwamba anaamini atarejea katika kiwango chake cha awali na kuweza kuisaidia vyema timu yake ili ifanikiwe kutetea ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa mara nyingine.

Hata hivyo amedai kuwa kwa sasa hana mpango wa kujiunga na timu yeyote licha ya baadhi ya timu kuhitaji huduma yake hii inatokana baada ya uongozi wa Yanga kukataa ombi la kutaka kumpeleka katika timu nyingine.

No comments