MAYANGA APANDISHA MMOJA KUTOKA TIMU YA VIJANA

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar umesema kwamba kwa sasa kocha mkuu wa klabu hiyo Salumu Mayanga amefanikiwa kumpandisha mchezaji Salehe Hamis kutoka timu ya vijana kwa ajili ya kumtumia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Afsa Habari wa Mtibwa Sugar,Tobiasi Kifaru amesema kwamba kocha Salumu Mayanga ameridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo chipukizi na ana imani ataisaidia vyema Mtibwa Sugar kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments