BARAZA LA WADHAMINI WA SIMBA LAKATAA MKUTANO MKUU

Baraza la wadhamini wa klabu ya Simba wamemuomba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda kusitisha mkutano mkuu wa klabu ya Simba uliopangwa kufanyika tarehe 11 ya mwezi wa 12 mwaka huu katika bwalo la maafisa wa Polisi Osterbey.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,mwenyekiti wa baraza hilo Hamisi Kilomoni amesema kwamba wameamua kufanya hivyo kwa kuwa uongozi umeshindwa kufuata taratibu za klabu hasa juu ya uitishwaji wa mkutano huo wenye lengo la kujadili mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa timu.

Katika hatua nyingine baraza hilo limeiomba taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU iwasaidie kufahamu juu ya taarifa za pesa za usajili za wachezaji Emmanuel Okwi na Mbwana Samata kwa kuwa fedha hizo hazikuingia kwenye akauni ya klabu na hazijulikani zilipo.

No comments