RAIS MAGUFULI KUWAKABIDHI SIMBA KOMBE LA UBINGWA

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli anatarajiwa kuikabidhi timu ya soka ya  Simba kombe la ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara katika mchezo wao dhidi ya Kagera Suger.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Rais wa TFF,Wallace Karia alisema kwamba TFF imemuomba waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amtaarifu Rais wa nchi juu ya swala hiko ikiwemo kupokea kombe la timu ya vijana ya Serengeti Boys ambayo imetwaa taji la ubingwa wa CECAFA.

"Tumeandika barua tumempelekea Mheshimiwa Waziri Mwakyembe ikiwezekana Rais akiona inapendeza Jumamosi tarehe 19 aweze kupokea kombe lile la wale vijana,na muheshimiwa Mwakyembe ameshaandika barua hiyo kumuomba Rais na amenihakikishia kuwa atafanya kila njia Rais atakubali"alisema Karia.

Karia alisema kwamba kwa kuwa Simba ilifanikiwa kuchukuwa kombe kabla ya ligi kwisha na ndio mchezo wa mwisho Simba kucheza nyumbani TFF imeona nivyema Rais nae akawepo ili kuwakabidhi kombe mabingwa hao.

Alisema kwamba dhamira yao ni kuweka karibu ushirikiano wa soka kati ya serikali na TFF ili kuleta tija ya maendeleo kwenye mchezo huo unaopendwa zaidi ulimwenguni.

No comments