RAIS MAGUFULI AKUBALI KUWAKABIDHI SIMBA KOMBE
Na Said Ally
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar hapo siku ya jumamosi.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Kaimu katibu mkuu wa shirikisho la soka hapa nchini TFF,Wilfred Kidao amesema kwamba taarifa ya kukubali kwa kiongozi huyo mkuu wa nchi kuwa mgeni rasmi imeelezwa na Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe.
Kidao alisema kwamba,wao kama TFF wamefurahishwa na jambo hilo la Rais kukubali wito wao kwani wanaimani ujio wake kwenye mchezo wa soka utaongeza ufanisi na maendeleo ya mchezo huo.
Alisema kwamba mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam unataraji kuanza kunako mishale ya saa 8:15 mchana kwa saa hapa nyumba huku kiingilio cha chini katika mpambano huo kikiwa ni shilingi elfu 2000.
Hata hivyo mbali ya kuwakabidhi Simba kombe la ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara pia Rais atapokea kombe la timu ya vijana ya Serengeti Boys ambayo imetwaa taji la ubingwa wa CECAFA.

Post a Comment