MAKONDA AWATAKA MASHABIKI KUUJAZA UWANJA WA TAIFA HAPO KESHO

Na,Said Ally
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaomba mashabiki wa soka hapa nchini kujitokeza kwa wingi hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara utakaowakutanisha Simba na Kagera Sugar.

Makonda alisema kwamba ujio wa Rais wa nchini katika mchezo huo utakaopigwa hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa ni mapinduzi makubwa katika soka.

Nae kaimu Rais wa klabu ya Simba Salm Abdalah,kwa upande wake ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika pambano hilo.

Mkuu wa idara ya Habari katika uongozi wa klabu ya Simba,Haji Manara yey alisema kwamba kwa upande wa kikosi maandalizi yameshakamilika kuelekea kwenye mchezo huo hivyo ni vyema mashabiki wakajitokeza kwa wingi hapo kesho.

No comments