WAZEE SIMBA WAUKATAA MKUTANO WA MABADILIKO YA KATIBA

Na, Said Ally
Wazee wanachama wa klabu ya Simba wamesema kwamba hawautambui mkutano wa dharula unaotarajiwa kufanyika siku ya jumapili 20/05/2018.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari Leo hii mratibu wa wazee wanachama wa klabu ya Simba Felex Makua alisema kwamba mkutano huo si halali kwa sababu viongozi ambao wanakaimu uongozi wameghushi katiba na kuidanganya serikali.

Makua alisema kwamba hakuna mkutano mkuu wowote ulioitishwa  na uongozi wa sasa zaidi ya ule wa tarehe 11/12/2016 wa kubadilisha katiba wakati wa akina Aveva.

Alisema kwamba maagizo ya serikali kupitia TFF ilikuwa  kufanya marekebisho ya katiba lkn hilo halikufanyika na badala yake viongozi wanaokaimu walijifungia ndani peke yao na kubadilisha vipengele takribani tisa bila ya kuitisha mkutano mkuu kama katiba ya klabu inavyoelekeza, hilo ni kosa la jinai la kughushi.

Aliongeza kwa kusema kuwa kwa mujibu wa katiba ya Simba mkutano wa dharula hauna mamlaka ya kubadilisha katiba kwa mujibu wa ibara ya 19 (4),hivyo wanautaka uongozi ufuate katiba ibara ya 22.3 vinginevyo klabu itaingia katika mgogoro mkubwa wa katiba jambo ambalo hawapendi litokee.

Uongozi wa klabu ya Simba ulitangaza mkutano wa dharula ambao utafanyika siku ya jumapili ya tarehe 20/05/2018, ukiwa ni mkutano wa mabadiliko ya katiba kuelekea kwenye mfumo wa Hisa.

No comments