NAIBU WAZIRI ASEMA SIMBA ITAIWAKILISHA VYEMA NCHI

Na,Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI ,Mh Joseph Kakunda, amefunguka kuhusiana na kikosi cha Simba kushiriki katika mashindano ya kimataifa akiamini kuwa timu hiyo itapeperusha vyema bendera ya taifa.

Kakunda ameeleza hayo leo Bungeni wakati akijibu  moja ya maswali ambayo wizara yake iliulizwa ambapo  alisema kuwa anaamini sasa wamepata mwakilishi mzuri kwenye michuano ya kimataifa, ambapo Simba watashiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Mabingwa hao wapya wa ligu kuu Tanzania bara kwa mwaka 2017/18 Simba SC wametinga bungeni Jijini Dodoma kwa mwaliko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge Mh Job Ndugai wakitambulishwa bungeni na mwenyekiti wa bunge Najma Murtaza Giga.

Simba wametwaaa ubingwa huo baada ya kuukosa kwa kipindi cha miaka mitano , mara ya mwisho kuwa mabingwa wa Tanzania ilikuwa msimu wa 2011/2012.

No comments