MASHABIKI SIMBA WAJIFARIJI LICHA YA KUFUNGWA


Baadhi ya mashabiki wa timu ya soka ya Simba wamesema kwamba licha ya kufungwa na Kagera Sugar katika mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa hakuwaondolei kufurahia ubingwa wao walioupata.

Mashabiki hao kwa nyakati tofauti wameiambia MWANDIKE BLOG kwamba kufungwa na Kagera Sugar si jambo geni kwao kwani adhma yao kuu ilikua kuchukua ubingwa ligi kuu ya Tanzania bara.

"Sisi tumefungwa na Kagera ksb kikosi kilichocheza sio kikosi kamili,si umeona John Bocco hakuanza hata baadhi ya wachezaji tegemezi hawakucheza Leo hii,kwa hiyo haikutushangaza"alisema Shabiki wa Simba.

Aidha alisema kwamba licha ya watani wao wa jadi Yanga kuwakabehi kwa kufungwa na Kagera Sugar hilo kwao halina mashiko,kwani wanapaswa kufahamu kua Simba ndio bingwa wa nchi kwa msimu huu.

Simba Leo hii imekabidhiwa kombe na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli katika uwanja wa Taifa ambapo Simba ilikubali kichapo cha bao 1-0.

No comments