MAGUFULI AWAPA NENO VIONGOZI WA SOKA

Na,Said Ally
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amevitaka vilabu vya soka hapa nchini pamoja na Tff kuhakikisha timu za Tanzania zinafanya vizur kwenye michuano ya kimataifa.

Magufuli ameyasema hayo uwanja wa Taifa akiwa mgeni rasmi katika pambano la ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar.

Alisema kwamba,Tanzania ni nchi kubwa hivyo ilipaswa timu zetu zifanye vizur kimataifa ili tuondoe msemo wa kichwa cha mwendawazimu.

Aliongeza kwa kusema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuinua michezo na kutambua hilo ndio maana ikaamua kujenga uwanja mkubwa wa michezo mkoani Dodoma.

No comments