SPORTPESA YAIPA SIMBA MILIONI MIA MOJA
Kampuni ya SportPesa leo hii imekabidhi hundi ya shilingi milioni 100 kwa mabingwa wapya wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Simba.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa SportPesa Tarimba Abbas alisema kwamba lengo la kuwakabidhi hundi hiyo ni kutimiza ahadi ambazo zimewekwa katika mkataba.
"Tunachokifanya leo ni kutimiza moja ya ahadi tuliyotoa wakati tunasaini mkataba mwezi mei mwaka jana kuwa tutatoa bonasi ya shilingi milioni 100 endapo mojawapo ya timu tunazozidhamini itachukua ubingwa wa ligi kuu,hivyo bila shaka timu ni Simba"alisema Tarimba.
Tarimba pia amewapongeza viongozi na wachezaji wa Simba kwa kufanikiwa kuwapa heshima kubwa wana Msimbazi kote nchini na kubwa zaidi ni kuwapa heshima wadhamini wa kikosi hicho kampuni ya SportPesa.
Nae kaimu Makamu wa Rais wa Simba Idd Kajuna,kwa niaba ya timu ameishukuru kampuni ya SportPesa kwa kuendelea kuwa nao bega kwa bega.
Kajuna alisema kwamba moja ya jambo ambalo Simba inajivunia msimu huu ni kuwa na mdhamini kama SportPesa ambae mbali na udhamini,pia wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kiuongozi.
Simba SC ni miongoni mwa timu nne kutoka Tanzania zitakazoshiriki kwenye michuano ya SportPesa Super Cup itakayofanyika nchini Kenya kuanzia juni 3-10 mwaka huu ikishirikisha timu nane kutoka nchi za Tanzania na Kenya.
Timu nyingine ni pamoja na Yanga,Singida United na JKU kutoka Tanzania sambamba na Gor Mahia,AFC Leopards,Kakamega Home Boys pamoja na Kariobangi Sharks kutoka nchini Kenya ambapo mbali na kuziloea kitita cha Dola 30,000 bingwa wa michuano hiyo ataenda nchini Uingereza kucheza dhidi ya Everton FC kwenye dimba la Goodison Park.
Post a Comment