DUSAN KONDIC NA ETIENN NDAYIRAGIJE MBIONI KURITHI MIKOBA YA KOCHA HANS

Na Said Ally
Kocha Etienne Ndayiragije ni miongoni mwa makocha wanaopewa nafasi ya kumrithi kocha Hans Van der Pluijm kwa ajili ya kuifundisha timu ya Singida United katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Mkurugenzi wa ufundi wa Singida United Festo Sanga ameiambia MWANDIKE BLOG,kuwa Ndayiragije ni miongoni mwa makocha ambao wamewasilisha maombi ya kutaka kuifundisha timu hiyo ya mkoani Singida.

Sanga alisema kwamba orodha ya makocha ambao wamewasilisha maombi ni kubwa tena wenye uzoefu wa kufundisha soka hapa nchini akiwemo kocha wa zamani wa Yanga Profesa Dusan Kondic na wengine waliwahi kuifundisha klabu ya Azam FC.
Alisema kwamba kwa sasa uongozi unaendelea kupitia CV za makocha hao na yule atakaeonekana anafaa kuifundisha timu hiyo basi uongozi hautasita kumtangaza kwa mashabiki na wapenda soka kwa ujumla.

Hata hivyo Sanga alisema kwamba swala la kocha Hans ambae anaalifiwa kujiunga na klabu ya Azam FC,uongozi utalitolea ufafanuzi baada ya kumalizika mechi ya fainali ya michuano ya FA itakayowakutanisha Singida United na Mtibwa Sugar june 2 mwaka huu huko mkoani Arusha.


No comments