YANGA IPO KAMILI KUIVAA MBAO FC

Na, Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuwakabili Mbao FC,hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Msemaji wa Yanga,Dismas Ten ameiambia MWANDIKE BLOG kwamba kila kitu kuelekea kwenye pambano hilo kipo vizuri na dhamira yao ni kupata ushindi kwenye mchezo huo licha ya kupitia kwenye changamoto nyingi.

Ten alisema kwamba kikosi kimerejea siku ya jana kikitokea mkoani Shinyanga na leo hii kimefanya mazoezi mepesi kikisubili mchezo huo.

Katika hatua nyingine Ten alisema kwamba kocha mkuu wa klabu hiyo Zahera Mwinyi Mkongomani amerejea nchini kwao Congo kwa ajili ya kuendelea na majukumu kwenye timu ya Taifa na baada ya hapo atarejea hapa nchini kuendelea na program mbalimbali katika kikosi cha Yanga.

No comments