KAULI YA SINGIDA UNITED BAADA YA KUWEPO TAARIFA ZA KOCHA HANS KUWAAGA VIONGOZI

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Singida United umekanusha taarifa zinazoelezwa na baadhi ya wadau kua  kocha mkuu wa klabu hiyo Hans Van der Pluijm amewaaga viongozi wa klabu kwa madai ya kuachana rasmi na timu hiyo ya mkoani Singida.

Katibu mkuu wa klabu hiyo Abdurahman Sima ameiambia MWANDIKE BLOG kuwa kwa upande wao kama uongozi hawana taarifa hizo ambazo zimeenea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Sima alisema kwamba taarifa hizo ni za mitandao kwani kocha huyo bado angali na mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kuifunidisha Singida United.

Alisema kwamba kocha huyo hawezi kuondoka bila ya kutoa taarifa kwa uongozi kwani mkataba wake una mbana kufanya hivyo kutokana na kusaliwa na kandarasi ya mwaka mmoja.

Aidha alisema kwamba,wao kama uongozi hawatakuwa na kikwazo cha kumruhusu kocha huyo kuondoka kule anapopahitaji lakini anapaswa kufuata taratibu husika ikiwemo sheria ya kuvunja mkataba.

No comments