MTIBWA SUGAR WAKUSANYA ALAMA 40

Goli alilofunga Hassan Dilunga katika dakika ya 81 katika mchezo wa jana lilitosha Mtibwa Sugar Sc kuibuka na pointi tatu muhimu dhidi ya Njombe Mji, mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Mchezo huo uliokuwa mkali wa aina yake kutokana na Mtibwa Sugar kupata upinzani mkali kutoka kwa Njombe Mji ambao walikuwa wanahitaji pointi tatu muhimu ili kujinusuru na janga la kushuka daraja lakini waka ambulia kipigo kutoka kwa Mtibwa Sugar.
Kipindi cha kwanza kilimalizika 0-0  , na kipindi cha pili Mtibwa Sugar walionekana kubadilika na kuhitaji ushindi kwa njia yoyote ile na wali ingia na njia ya kupiga mashuti ya mbali  kufanikiwa kufunga goli.
Pointi tatu za jana zimewafanya Mtibwa Sugar Sc kufanikiwa kukusanya pointi 40 katika michezo 29  ya ligi kuu bara (Vodacom Premier League).
Wana tam tam wamebakiza mchezo mmoja ili kumaliza msimu huu kwa upande wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) na mchezo huo utakuwa dhidi ya Mbeya City Fc utachezwa May  28 katika dimba la Manungu Complex.

No comments