NAHODHA YANGA AELEZA SABABU ZILIZOWAONDOSHA KLABU BINGWA

Nahodha wa timu ya soka ya Yanga Nadri Haroub amesema kwamba kikosi cha timu yake kimeshindwa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika kwa sababu wameshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani.

Nadri alisema kwamba katika mechi ya jana dhidi ya Township Rollers iliyomalizika kwa sale tasa kikosi chake kilicheza vizur lkn matokeo ya kufungwa nyumbani 2-1 ndio yaliyowapa wakati mgumu.

"Siku zote kwenye michuano hii ya kimataifa inatakiwa uutumie vyema uwanja wa nyumbani,sasa sisi tumeshindwa kufanya hivyo" alisema Nadri.

Aidha alisema kwamba kwa Sasa wanaelekeza nguvu zao katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambako timu hiyo imeangukia na ana imani huko watafanya vizuri.

Yanga imeondoshwa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika kwa magoli ya jumla 2-1 yaliyofungwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na timu hiyo ya Township Rollers ya nchini Botswana.

No comments