MSUVA KUIONGOZA DIFAA HASSAN EL JADIDI KUIKABILI AS VITA

Winga wa zamani wa timu ya soka ya Yanga Saimon Msuva Leo hii atakuwa na kazi kubwa ya kuiwezesha timu yake ya Difaa Hassan El Jadidi kutinga katika hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika.

Difaa Hassan El Jadidi Leo hii itakuwa ugenini kumenyana na As Vita ya nchini Congo mchezo unaotarajiwa kupigwa kunako mishale ya saa 10 :30 jioni kwa saa za hapa nyumbani.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Morocco March 7 mwaka huu Difaa Hassan El Jadidi ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 goli ambalo lilifungwa na Saimon Msuva hivyo Leo hii watakuwa na kazi kubwa ya kulinda ushindi huo.

No comments