CHIRWA,TSHISHIMBI NA MAKAPU KUIKOSA MECHI YA SHIRIKISHO

Na Said Ally
Wachezaji watatu wa timu ya soka ya Yanga,Obrey Chirwa,Papy Tshishimbi na Said Makapu watakosekana katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika baada ya ratiba ya kombe hilo kupangwa hapo kesho

Msemaji wa timu ya Yanga Dismas Ten amesema kwamba wachezaji hao watakosekana katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo baada ya wachezaji hao kuzawadiwa kadi za njano katika ushiriki wa michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika.

Ten alisema kwamba ni vyema watanzania wakafahamu swala hilo kwa kuwa sio jambo la kificho hasa katika maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

Alisema kwamba kwa sasa wachezaji wamepewa mapumziko ya siku kadhaa kabla ya kurejea siku ya alhamisi kuendelea na maandalizi ya michezo yao inayowakabili ikiwemo mechi ya FA dhidi ya Singida United.

Yanga inataraji kushiriki michuano ya kombe la shirishikisho barani Afrika baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika na timu ya Township Rollers ya Botswana.

No comments