KAULI YA MSUVA BAADA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI YA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA

Mchezaji wa Tanzania anaecheza soka la kulipwa nchini Morocco Saimon Msuva amewataka watanzania kumuombea ili aweze kufanya vizur katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Msuva ameyasema hayo baada kuiwezesha timu yake ya Difaa Hassan El Jadidi kufuzu katika hatua ya makundi kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Alisema kwamba kucheza kwake kwenye hatua ya makundi kutamfanya aonekane zaidi na mawakala wa wachezaji jambo ambalo anaamini linaweza kumpa mwanga wa kusajiliwa na vilabu kutoka nchi za Ulaya.

Timu ya Difaa Hassan El Jadidi imefanikiwa kutinga hatua ya makundi klabu bingwa barani Afrika baada ya kupata sale ya 2-2 ugenini dhidi ya As Vita ya Congo kufuatia ushindi wa awali wa bao 1-0.

No comments