MWANZA WAPANGA KUUREJESHA MCHEZO WA VOLLEYBALL

Na, Mwandishi Wetu
Mashindano ya Merijam Volleyball Championship yanataraji kuanza rasmi hapo kesho huko mkoani Mwanza kwa timu mbalimbali kutoka Tanzania bara na visiwani kushindana katika shindano hilo.

Mratibu wa mashindano hayo kutoka katika chama cha Volleyball mkoani Mwanza Majaliwa Peter Mayunga ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kwa upande wao kama chama maandalizi yako vizuri kuelekea kwenye mashindano hayo yanatarajiwa kufika tamati march 25 mwaka huu.

Mayunga alisema kwamba mashindano hayo ni mazuri na nia yao ni kurejesha heshima ya Volleyball mkoani Mwanza kama ilivyokuwa awali ambapo mchezo huo ulikuwa na hamasa zaidi kuliko mpira wa miguu.


No comments