MAYANGA AKANUSHA TAARIFA ZA MITANDAONI

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Salum Shabani Mayanga amekanusha taarifa zinazoendelea kuenea kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa yeye hakuhusika katika uchaguzi wa timu ya Taifa iliyokwenda nchini Algeria kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye tarehe za kalenda ya FIFA.

Mayanga amesema kwamba taarifa inayozunguka mitandao sio taarifa sahihi bali ni upotoshaji wenye nia ya kuwavuruga.

"Watu waache kupotosha umma mimi ndio nimechaguwa kikosi chote kilicho safiri kwenda Algeria na si vinginevyo,kocha Hemed Morroco nilimuachia jukumu la kutangaza kikosi  baada ya uteuzi"alisema Mayanga.

Stars jana ilishindwa kufuta uteja mbele ya timu ya Algeria katika mchezo wa kirafiki uliochezwa nchini Algeria baada ya kukubali kufungwa kwa jumla ya magoli 4-1.

No comments