DONALD NGOMA AREJEA KIKOSINI YANGA

Na Said Ally
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Yanga,Donald Ngoma anataraji kuanza mazoezi na wenzake siku ya alhamisi kwa ajili ya maandalizi ya kujiwinda na michuano mbalimbali inayowakabili ikiwemo mechi ya FA dhidi ya Singida United.

Msemaji wa timu ya soka ya Yanga,Dismas Teni amesema kwamba Ngoma ni miongoni mwa wachezaji watakaoanza mazoezi siku ya alhamisi baada ya kuonekana yuko vizuri kupitia lipoti ya daktari na maelezo ya mwenyekiti wa kamati ya mashindano.

Ten alisema kwamba Ngoma alishaanza mazoezi mepesi kabla ya kuanza mazoezi hayo na wachezaji wenzake ambao wamepewa mapumziko ya siku kadhaa baada ya kutoka kwenye ushiriki wa mchezo wa kombe la klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana.

Hata hivyo Dismas ametoa angalizo kwa mashabiki na wanachama kuwa licha ya kuanza mazoezi kwa mchezaji Donald Ngoma lakini sio kigezo cha yeye kuanza kucheza mechi,kwani taratibu za kucheza zinapangwa na benchi la ufundi kutokana ubora wa mchezaji.

No comments