HAWA NDIO WAPINZANI WA YANGA KWENYE KOMBE LA SHIRIKISHO

Timu ya soka ya Yanga Imepangwa na timu ya Wolaitta Dicha kutoka nchini Ethiopia katika mchezo wa mtoano wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Yanga itaanzia nyumbani katika mchezo wa awali unaotarajiwa kuchezwa April 6,7na 8 mechi inayotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Ratiba hiyo bila Shaka inawaondoa wasiwasi mashabiki wa Yanga ambao wengi wao walizani kwamba huenda kikosi hicho kingekutana na timu za kiarabu.

Wapinzani hao wa Yanga wamefanikiwa kufika hapo baada kuiondosha timu ya Zimamoto ya Zanzibar pamoja na timu ya Zamalek ya nchini Misri ambapo kwa sasa wanashika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi nchini Ethiopia.

No comments