MECHI YA NJOMBE MJI NA SIMBA BADO HAIJAPANGIWA TAREHE

Na Said Ally
Bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara imekanusha taarifa zinazoeleza kuwa bodi hiyo imeshapanga tarehe ya mchezo wa kiporo kati ya Njombe Mji na Simba.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniphace Wambura ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kuwa hadi Sasa hawajapanga ratiba ya mechi hiyo ya kiporo kama inavyoelezwa na baadhi ya watu kuwa itachezwa April 3 mwaka huu.

Wambura alisema kwamba bodi ya ligi inataraji kukaa siku ya jumatatu kupanga tarehe za mechi hizo za viporo ikiwemo mchezo utakaowakutanisha Simba na Yanga hivyo ni vyema wadau wa soka wakazipuuzia taarifa hizo ambazo hazina ukweli.

No comments