KISONGO AMPA NAFASI KUBWA NDEMLA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA

Wakala wa wachezaji anaetambulika na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA,Jamali Kisongo amesema kwamba mchezaji wa timu ya soka ya Simba Said Hamis Ndemla anaendelea vyema na majalibio yake nchini Sweden kwa ajili ya kusaka nafasi ya kucheza soka la kulipwa.

Kisongo alisema kwamba kwa mujibu wa taarifa ambazo amezipata kutoka kwa mwalimu wa timu hiyo ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden zinaonyesha Ndemla ana nafasi kubwa ya kufuzu kwenye majalibio hayo.

Kisongo amewataka watanzani kuwa na subra kwa kipindi na kumuombea dua mchezaji huyo ili afanikiwe malengo yake ya kucheza soka la kulipwa.


No comments