MBEYA CITY WAKO TAYARI KUWAVAA SINGIDA UNITED

Kikosi cha Mbeya City FC kimewasili mjini Singida siku ya alhamisi tarehe 23.11.17 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo nambari 82 wa jumamosi (25.11.17) dhidi ya Singida United. Kikosi hiko kiliendelea na mazoezi katika viwanja vya Jordan na Highland Camp huko Morogoro.
Mchezo huo utakua ni mchezo wa kwanza kwa timu hizo kukutana mara baada ya Singida United kupanda daraja msimu huu wa 2017/2018 ambapo kwa mujibu msemaji wa timu ya Mbeya City Shah Mjanja amesema kwamba kikosi chao kipo tayari kwa mapambano.
Mara baada ya mchezo huo timu ya Mbeya City itarejea nyumbani kupisha mapumziko ya Kilimanjaro Heros itakayoshiriki mashindano ya Chalenji huko Kenya.
Mchezo unaofuata baada ya Singida United kwa upande wa Mbeya City ni dhidi ya Kagera Sugar, mchezo wa ligi nambari 90 katika dimba la Sokoine.

No comments