KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI YA TFF YATOA TAMKO ZITO KWA TIMU ZA LIGI

Mwenyekiti wa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji wa shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,Elias Mwanjala amevitaka vilabu nchini kuwapatia barua wachezaji wao iwapo wamebainika kumaliza mikataba ili waweze kusajiliwa na vilabu vingine ambavyo vinawahitaji.

Mwanjala alisema kwamba vilabu vingi vya vimekuwa na tabia ya kushindwa kuwapa barua ya kuwa huru wachezaji waliomaliza mikataba yao jambo ambalo linawapa wakati mgumu wachezaji hao.

Aidha alisema kwamba klabu zinapaswa kufahamu kuwa kama zitashindwa kumlipa mchezaji mshahara wake ndani ya miezi mitatu basi klabu hiyo imevunja mkataba na wao watakuwa huru kumuidhinisha katika timu nyingine atakayohitaji kwenda.


No comments