PAMBANO LA YANGA NA PRISON LAFANYIWA MABADILIKO YA UWANJA

Bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara imefanya mabadiliko ya uwanja katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Yanga na Tanzania Prisons,mchezo uliopangwa awali kuchezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam siku ya jumamosi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba wamepokea taarifa kutoka kwenye uongozi wa bodi ya ligi juu ya mabadiliko hayo ya uwanja kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Prisons.

Dismas alisema kwamba mchezo huo sasa utachezwa kwenye uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi siku ya jumamosi baada ya uwanja wa Uhuru kutumika kwa matumizi mengine ya kijamii tarehe 24 hadi tarehe 26 mwezi huu.

No comments