LIPULI FC YAMTAKA MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA SIMBA

Timu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa iko mbioni kufanya usajili wa mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba Fredrick Blagnon kutoka nchini Ivory Coast ili aweze kukiongeza nguvu kikosi cha timu hiyo kwenye ushiriki wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Kocha mkuu wa timu hiyo Sleiman Matola amesema kwamba katika taarifa yake ambayo ameiwasilisha kwa uongozi wa timu ya Lipuli imeeleza mahitaji ya mchezaji huyo ambae anaamini kama atasajiliwa basi atakuwa msada wa kutosha.

Matola alisema kwamba ameshafanya maongezi na mchezji huyo na mwenyewe ameridhia kujiunga na timu hiyo ya Lipuli.

Alisema kwamba mipango yake katika dirisha dogo hili la usajili linaloendelea sasa ni kuongeza wachezaji kwenye safu ya ushambuliaji kwani eneo hilo limekuwa likuyumba kwa kutokuwa na wachezaji muhimu kwenye sehemu hiyo.

Hata hivyo Matola ameonyesha wasiwasi kwa uongozi wa klabu hiyo kwani anaamini huenda wakashindwa kutimiza mahitaji hayo kutokana na klabu kutokuwa na kipato kizuri cha uendeshaji wa timu.

No comments