TP MAZEMBE WAANZA VYEMA FAINALI YA SHIRIKISHO

TP Mazembe imeanza vema fainali ya kuwania taji la Shirikisho barani Afrika baada ya kuishinda SuperSport United ya Afrika Kusini kwa mabao 2-1.
Hata hivyo TP Mazembe bado wana kazi kubwa ya kufanya katika mchezo wa fainali ya pili itakayopigwa nchini Afrika ya Kusini kwani licha ya kufungwa kwa goli hizo mbili lakini SuperSport United walionyesha ushindani wa hali ya juu.
Fainali ya pili itachezwa tarehe 25 mwezi huu.

No comments