JANG'OMBE BOYS WARIDHISHWA NA MICHUANO YA SPORTPESA

Kocha mkuu wa timu ya Jang'ombe Boys Mahmood Abdalah Yossof alisema kwamba licha ya kuondoshwa kwenye michuano ya SportPesa katika hatua ya awali lakini anaamini amepata la kujifunza

Mahmood alisema kwamba anaamini vijana wake walijituma Zaidi kwenye mechi yao dhidi ya kwanza dhidi ya Gor Mahia lakini bahati haikuwa yao hivyo kwa sasa wanaelekea Zanzibar kwa ajili ya kuendelea na ligi kuu ya huko huku pia akiamini atakwenda kuyafanyia kazi mapungufu ambayo ameyaona kupitia mashindano hayo ya SportPesa.


Alisema kwamba mashindano hayo ni mazuri na yamewapa funzo kwa upande wao hivyo akiwa kama kocha mkuu wa timu hiyo ya Jangombe atahakikisha mbinu ambazo amezipata kutoka kwa wenzake basi atazielekeza kwenye kikosi chake kwa maboresho zaidi.

Jang'ombe Boys imeondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya kukubali kufungwa kwa jumla ya magoli 2-0 na timu ya Gor Mahia kupitia kwa mshambuliaji wake Meddy Kagere.

No comments