SIMBA WAVUNJA KAMBI RASMI

Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya SportPesa,uongozi wa timu ya Simba umevunja kambi rasmi na kuamua kuwapa mapumziko wachezaji kabla ya kurejea kwa mara nyingine kujiwinda na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Makamu wa rais wa Simba,Geofrey Nyange Kaburu ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba mapumziko hayo hayawatahusu viongozi kwani kwa upande wao bado wanaendelea na mchakato wa usajili na maswala mbalimbali yanayohusiana na klabu.

Kaburu alisema kwamba kwa sasa uongozi ushafanikiwa kukamilisha usajili wa wachezaji wawili ambao ni Jamali Mwambeleko kutoka timu ya Mbao FC pamoja na Yusuf Mlipili ambao hapo jana walionekana kwenye kikosi cha Simba kilichocheza dhidi ya timu ya Nakuru All Stars.

Alisema kwamba hata swala la mchezaji Emanuel Okwi kama lipo kwenye mapendekezo ya mwalimu basi uongozi utalifanyia kazi kupitia kamati yake ya usajili inayongozwa na Zakaria Hans Pope.

No comments