STARS YAREJEA KWA KUJIAMINI

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo hii kimerejea hapa nchini kikitokea Misri ambapo kiliweka kambi maalum kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika AFCON dhidi ya Lethoto.

Kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga alisema kwamba maandalizi yao ndani ya siku saba wakiwa nchini Misri yamekuwa mazuri na yatawasaidia kufanya vyema kwenye mechi yao hiyo itakayopigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Mayanga alisema kwamba kwenye pambano hilo watamkosa mchezaji Mohamed Hussein anaemudu kucheza vizuri beki namba tatu baada ya kuwa majeruhi aliyoyapata kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA iliyowakutanisha Simba na Mbao FC.

No comments