SIMBA WAIPANIA MICHUANO YA SPORTPESA

Uongozi wa timu ya Simba umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimejiandaa vyema kufanya vizuri kwenye michuano ya SportPesa inayotaraji kuanza kutimua vumbi siku ya kesho

Mratibu wa timu ya Simba,Abas Ally alisema kwamba wachezaji wote ukiwaacha wale ambao wamejiunga na timu za Taifa tayari wameanza mazoezi toka siku ya ijumaa kwa ajili ya kujiwinda na michuano hiyo inayotaraji kuwa na ushindani wa hali juu.

Abasi alisema kwamba benchi la ufundi linataraji kuwatumia wachezaji ambao hawakupata nafasi kwenye ushiriki wa ligi kuu ya Tanzania bara ambao anaamini wataipa mafanikio ya kuwa mabingwa.

Alisema kwamba katika michuano hiyo benchi la ufundi limepanga kuwatumia wachezaji ambao hawakupata nafasi kwenye michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara ili kubaini viwango vyao.

No comments