HATMA YA MSIMAMO WA MANJI KUJULIKANA KESHO

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Clement Sanga hapo kesho mishale ya saa tano asubuhi anataraji kuzungumza na viongozi wa matawi wa klabu hiyo ili kujadili maswala mbalimbali ya klabu ikiwemo swala la kujiuzulu kwa Yusuf Manji.

Makam mwenyekiti wa matawi ya Yanga Bakili Makele amikili kupata taarifa hiyo huku akiwahimiza viongozi wa matawi ya klabu hiyo kujitokeza kwa wingi klabu hapo ili kufahamu yale atakayoyazungumza makamu mwenyekiti.

Sanga katika mkutano huo imeelezwa mbali na swala hilo la Manji pia atazungumzia swala la mkataba wa SportPesa juu ya kile kilichopo kwenye mkataba huo pamoja na kuzungumzia maswala ya zoezi la usajili ndani ya klabu hiyo.

No comments