KOCHA WA GOR MAHIA ATAMBA KUWA BINGWA WA MICHUANO YA SPORTPESA

Wakati michuano ya SportPesa ikitarajiwa kufika tamati hapo kesho,kocha wa timu ya Gor Mahia Zedekiah Otieno amesema kwamba kikosi chake kimejipanga vyema kuwakabili AFC Leopard katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Otieno alisema kwamba wanaingia kwenye fainali hiyo wakitambua kuwa mechi itakuwa ngumu zaidi kutokana na ushindani uliopo kwa timu hizo kutoka nchini Kenya lakini kwao wamejipanga kupambana.

Alisema kwamba mechi hiyo itakuwa nzuri kwa pande zote kwani watacheza mchezo huo pasipo presha yeyote ya mashabiki kama inavyokuaga nchini Kenya pindi mahasimu hao wanapokutana hivyo hali hiyo itawaweka huru wachezaji kuonyesha umahili wao.

No comments