WAZIR JUNIOR ASEMA HAYA BAADA YA KUJIUNGA NA AZAM FC

Baada ya kusajiliwa na klabu ya Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili mchezaji Waziri Junior amesema kwamba yeye amefarijika kujiunga na klabu hiyo kwani alikuwa na ndoto za kuitumikia timu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Chamazi katika safari yake ya soka.

Junior alisema kwamba anaamini Azam itakuwa njia ya safari yake ya kufika kule anapopahitaji akiamini kuwa atajifunza mengi Zaidi kupitia klabu hiyo.

Alisema kwamba vilabu vingi vilikuwa vinahitaji huduma yake lakini yeye ameona Azam ni mahali sahihi kwa upande hasa katika azma yake ya kusonga mbele katika medali ya soka.

Aidha Waziri alizungumzia swala la yeye kuonekana kwake katika klabu ya Yanga akiwa na baadhi ya kiongozi wa klabu hiyo ambayo pia nayo ilikuwa na mpango wa kumsajili.

Alisema kwamba kuonekana kwake Yanga si jambo la ajabu kwani wachezaji wengi wamekuwa wakifanya hivyo lakini kwake amefanya maamuzi ya kutosaini Yanga na kuamua kujiunga na Azam FC.

Mchezaji huyo sasa rasmi atatumia jezi namba saba ambayo ndani ya Azam ilikuwa haina mchezaji aliyekuwa anaitumia na mwenyewe amejinasibu kuitendea vyema jezi hiyo.

No comments