KOCHA WA NAMUNGO NA MSIMAMIZI WA KITUO WAPIGWA

Wakati kukiwa na taarifa kuwa kocha wa timu ya Namungo ya mkoani Lindi inayoshiriki ligi daraja la pili pamoja na msimamizi wa kituo wamepigwa na wanaosadikiwa ni mashabiki na viongozi wa timu ya Might Elphant kwa kitendo kinachodaiwa kukutwa wakifanya Imani za kishirikina kwenye uwanja wa mechi hapo jana,leo hii kocha mwenyewe wa Namungo amesema kwamba taarifa za kupigwa kwake ni za kweli lakini yeye hakukutwa akifanya jambo hilo.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,kocha Mahadi Zulfkr amesema kwamba yeye ameshangwazwa na watu hao ambao wamemfanyia vurugu hizo za kumpiga kwa kuwa yeye hakufanya jambo hilo Zaidi ya watu hao kumfuata nyumbani na kuanza kumpleka uwanja huku wakimpiga.

Kwa upande wake msimamizi wa kituo cha Nachingwea mkoani Lindi ambao ndio uwanja wa timu ya Namungo,amesema kwamba katika tukio hilo Namungo hawahusiki kwa lolote kwani wao si wahusika wa jambo hilo na yeye pia ameshangwazwa na kitendo cha kupigwa kwake.

Amesema kwamba yeye aliingia uwanjani baada ya kupata taarifaa kuwa ndani ya uwanja kuna mtu anapigwa pasipo kufahamu sababu ya tukio hilo,na kwa kuwa yeye ndie msimamizi wa kituo ndipo alipoamua kwenda kushuhudia jambo hilo.



No comments